Mark Elliot Zuckerberg (amezaliwa 14 Mei 1984) ni mjasiriamali Mmarekani anayejulikana kama mwanzilishi mwenza wa tovuti maarufu ya urafiki mtandao ya Facebook. Zuckerberg alianzilisha Facebook pamoja na wanafunzi wenzake Dustin Moskovitz, Eduardo Saverin, na Chris Hughes wakati wakihudhuria Chuo Kikuu cha Harvard. Zuckerberg ndiye Afisa Mkuu Mtendaji wa Facebook.[2] Amekuwa mada ya utata kuhusu asili ya biashara yake. [3]